Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha

( AUWSA )

RAIS SAMIA ABADILI HISTORIA YA CHANGAMOTO YA MAJI MONDULI

Imewekwa: 13 November, 2023
RAIS SAMIA ABADILI HISTORIA YA CHANGAMOTO YA MAJI MONDULI

RAIS SAMIA ABADILI HISTORIA YA CHANGAMOTO YA MAJI MONDULI

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (MB) ameshuhudia Hafla ya utaiji saini wa Ujenzi wa mradi wa maji kutoka Mradi mkubwa wa Maji Jiji la Arusha kwenda Vijiji 13 pamoja na ujenzi wa mradi wa Maji Katika vijiji 4 ambapo gharama ya Miradi hiyo ni shilingi za Kitanzania Bilioni 27 zilizotewa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.

Vijiji hivyo 17 vitakavyo nufaika na Miradi hiyo ni Meserani, Meserani Bwawani, Engorika, Engiloriti, Naalarami, Arkatani, Mtimmoja, Arkaria, Nanja, Lepurko, Eng’aroj, Losimingor, Mbuyuni, Makuyuni, Naiti, Mbuyuni na Losimingor.

Aidha kabla ya tukio hilo Waziri Aweso amefika na kujionea changamoto ya Maji kwa wananchi wa kijiji la Lepurko na kuagiza kazi ya ujenzi wa Bwawa kuanza mara moja jumatatu na kuelekeza Milion 248 kutengwa ili kufanikisha kazi hii ndani ya kipindi ch mwezi mmoja.