Utaratibu wa Maunganisho Mapya
Utaratibu wa Maunganisho Mapya
Imewekwa: 14 November, 2023
UTARATIBU WA MAUNGANISHO MAPYA
1. Fomu ya maombi
- Mteja anapaswa kujaza fomu ya maombi ambayo inapatikana bure ofisi kuu ya AUWSA, kwenye tovuti ya AUWSA na kutoka ofisi zote za kanda.
- Fomu iwe na mhuri kutoka ofisi ya Mtendaji au Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa.
2. Viambatisho vinavyohitajika
- Barua ya Afisa Mtendaji au Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa eneo husika
- Picha mbili (Passport Size)
- Nakala ya kitambulisho (Kitambulisho cha Taifa, Kadi ya Mpiga kura, Leseni ya udereva ama kitambulisho kingine kinachotambulika na serikali)
- Kwa taasisi/mashirika watapaswa kupiga muhuri sehemu ya picha na kuweka viambatisho vya usajili wa taasisi/mashirika yao.
3. Upimaji (Survey)
- AUWSA itafanya upimaji kwa mteja aliyekamilisha kujaza fomu ya maombi na viambatisho vinavyohitajika na kuiwasilisha ofisi za AUWSA ndani ya siku saba za kazi.
4. Makadirio ya Gharama
- AUWSA itaandaa gharama zote za makadirio zinazohitajika kwa ajili ya maunganisho mapya.
- Ununuzi wa vifaa vipya vya kuunganisha huduma ya maji itafanywa na AUWSA kwa kufuata sheria na kanuni za manunuzi ya umma.
5. Taarifa kwa mteja.
-
Baada ya makadirio ya gharama, AUWSA itamjulisha mwombaji kupitia ujumbe mfupi (SMS) jumla ya gharama ya maunganisho. Gharama hizi pia zitapatikana kwa mteja kufika ofisi za AUWSA.
6. Malipo
- Makadirio ya gharama yatalipwa na mteja kupitia namba ya malipo ya serikali – Control Number, au utaratibu utakaowekwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
7. Utekelezaji wa maunganisho mapya.
- Baada ya mteja kukamilisha malipo ya gharama za maunganisho mapya AUWSA itamfanyia mteja maunganisho ya huduma ya majisafi.
- Baada ya maunganisho kukamilika AUWSA itafanya majaribio ya kuhakiki ufanisi wa maunganisho.
- Dira ya maji itafungwa kwa mteja bure.