Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha

( AUWSA )

MRADI WA MLANGARINI WAENDELEA KWA KASI

Imewekwa: 16 April, 2024
MRADI WA MLANGARINI WAENDELEA KWA KASI

KAZI YA ULAZAJI BOMBA MRADI WA MLANGARINI IKIENDELEA

14 Aprili 2024

Ulazaji wa Bomba za Majisafi za zipenyo tofauti ukiendelea katika mradi wa Majisafi Mlangarini ambapo inatarajiwa kulazwa zaidi ya Kilometa 65, kazi hiyo inayofanywa na Mkandarasi ZONGII CONTRACTOR CO LIMITED inatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 2024

Mradi huo utakao wanufaisha wananchi zaidi ya 12000 wa kata za Moivaro na Mrangarini unagharimu kiasi cha Tzs Bilioni 3.6 ambapo itajumuisha ujenzi wa Tank la lita za ujazo 500000 ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji urefu wa km 65