OFA YA KUREJESHEWA HUDUMA YA MAJISAFI BILA GHARAMA (RECONNECTION FEE)
OFA YA KUREJESHEWA HUDUMA YA MAJISAFI BILA GHARAMA (RECONNECTION FEE)
Imewekwa: 17 March, 2026
Katika kuadhimisha wiki ya Maji Tarehe 16-22 Machi 2026, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha imetoa OFA kwa kila mteja ambaye amesitishiwa huduma ya Majisafi, kurejeshewa huduma hiyo bila gharama (reconnection fee). Fika ofisi za Auwsa zilizopo katika eneo lako kwaajili ya kuhudumiwa. OFA HII NI KUANZIA TAREHE 16 - 31 MACHI 2026