Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha

( AUWSA )

Utaratibu wa Maunganisho Mapya

Imewekwa: 14 November, 2023
Utaratibu wa Maunganisho Mapya

UTARATIBU WA MAUNGANISHO MAPYA

 1. Fomu ya maombi

 • Mteja anapaswa kujaza fomu ya maombi ambayo inapatikana bure ofisi kuu ya AUWSA, kwenye tovuti ya AUWSA na kutoka ofisi zote za kanda.
 • Fomu iwe na mhuri kutoka ofisi ya Mtendaji au Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa.

2. Viambatisho vinavyohitajika  

 • Barua ya Afisa Mtendaji au Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa eneo husika
 • Picha mbili (Passport Size)
 • Nakala ya kitambulisho (Kitambulisho cha Taifa, Kadi ya Mpiga kura, Leseni ya udereva ama kitambulisho kingine kinachotambulika na serikali)
 • Kwa taasisi/mashirika watapaswa kupiga muhuri sehemu ya picha na kuweka viambatisho vya usajili wa taasisi/mashirika yao.

3. Upimaji (Survey) 

 • AUWSA itafanya upimaji kwa mteja aliyekamilisha kujaza fomu ya maombi na viambatisho vinavyohitajika na kuiwasilisha ofisi za AUWSA ndani ya siku saba za kazi.

4. Makadirio ya Gharama  

 • AUWSA itaandaa gharama zote za makadirio zinazohitajika kwa ajili ya maunganisho mapya.
 • Ununuzi wa vifaa vipya vya kuunganisha huduma ya maji itafanywa na AUWSA kwa kufuata sheria na kanuni za manunuzi ya umma.

5. Taarifa kwa mteja. 

 • Baada ya makadirio ya gharama, AUWSA itamjulisha mwombaji kupitia ujumbe mfupi (SMS) jumla ya gharama ya maunganisho. Gharama hizi pia zitapatikana kwa mteja kufika ofisi za AUWSA.

6. Malipo 

 • Makadirio ya gharama yatalipwa na mteja kupitia namba ya malipo ya serikali – Control Number, au utaratibu utakaowekwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

7. Utekelezaji wa maunganisho mapya.

 • Baada ya mteja kukamilisha malipo ya gharama za maunganisho mapya AUWSA itamfanyia mteja maunganisho ya huduma ya majisafi.
 • Baada ya maunganisho kukamilika AUWSA itafanya majaribio ya kuhakiki ufanisi wa maunganisho.
 • Dira ya maji itafungwa kwa mteja bure.