Malalamiko Ya Wateja
MAONI NA MALAMIKO YA WATEJA
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira AUWSA inapokea maoni na kushughulikia malalamiko kuhusu utoaji wa huduma. Mteja anaweza kuwasilisha malalamiko yake kwa kutumia njia zifuatazo:
- Kufika Ofisi za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira zilizopo Arusha Mjini pamoja na ofisi za kanda zilizopo Moshono, Lemara na Murieti.
- Kuandika barua pepe kupitia ( md@auwsa.go.tz ).
- Au kwa kupiga simu kupitia Kituo cha huduma kwa wateja kwa namba ya bure 0800110069
- Namba ya WhatsApp 0734200288
UTARATIBU WA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA WATEJA
Malalamiko yote yatasikilizwa na kutatuliwa ndani ya siku 5 za kazi. Endapo mlalamikaji hataridhika na majibu yatakayotolewa na Mamlaka, anaweza kukata rufaa Mamlaka yaUdhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa kufuata taratibu zilizoainishwa kwenye Sheria ya EWURA Sura 414, na Kanuni za EWURA za kuandaa na kuwasilisha malalamiko.
WASILISHA LALAMIKO LAKO KUPITIA:
Anuani: S.L.P 13600, ARUSHA
Simu ya huduma kwa wateja : 0800110069 bure
Barua Pepe: md@auwsa.go.tz
Tovuti: www.auwsa.go.tz
WhatsApp: 0734200288
Simu ya Ofisi: +255 27-2547186