Mwenge wa Uhuru watembelea na kukagua mradi wa maji Mirerani.
Mwenge wa Uhuru watembelea na kukagua mradi wa maji Mirerani.
Imewekwa: 13 July, 2026
Tarehe 12.07.2026 Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2026 Ndugu Wazo Michael Mwang'onda ametembelea na kukagua mradi wa Maji Mirerani,mradi ambao ni sehemu ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji wa Jiji la Arusha.
Mradi huo unaojengwa kwa fedha kutoka Serikali kuu,unajengwa kwa ya gharama ya Shilingi za Kitanzania bilioni 4.3 ambapo kiasi cha Shilingi za Kitanzania 2.5 bilioni zimeshatumika kujenga mradi huo.
Jumla ya wakazi elf 57,000 watanufaika na mradi huo kutoka kata za Mirerani,Endiamtu,Naisinyai na Shambarai.
Viongozi na wananchi wa maeneo yanayonufaika na mradi wanashukru Serikali kwa kumtuma mama ndoo kichwani na kufurahi kupata majisafi na salama ambayo hawajawahi kuyapata toka Tanzania ipate uhuru.