Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha

( AUWSA )

Karibu

Justine G. Rujomba photo
Mhandisi. Justine G. Rujomba
Mkurugenzi Mtendaji

: md@auwsa.go.tz

: +255 272547186/ 2547163

Ninafurahi kuwakaribisha kwenye tovuti ya Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA), tovuti inayoelezea kwa kina kazi mbalimbali zinaofanywa na Mamlaka hii, maeneo tunayoyafikia, huduma za maji, maji taka, miradi mbalimbali inayoendelea na jitihada za kuboresha maji na usafi wa mazingira.

Tovuti hii, imetayarishwa kutoa taarifa, mwongozo na majibu kwa masuala yanayohusiana na AUWSA. Pia unaweza kujiunga na Mitandao yetu ya Kijamii, ambapo wadau wetu wanaweza kuwasiliana vizuri na AUWSA. Kujiunga na mitandao hiyo, tafadhali tumia kiungo kilichopo chini ya ukurasa huu.

Nawakaribisha wote mtumie tovuti hii kuwasiliana na AUWSA.

 

Mha. Justine G. Rujomba