Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha

( AUWSA )

KAMATI YA BUNGE MAJI NA MAZINGIRA YARIDHISHWA NA UTENDAJI WA AUWSA

Imewekwa: 21 August, 2024
KAMATI YA BUNGE MAJI NA MAZINGIRA YARIDHISHWA NA UTENDAJI WA AUWSA

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso akiambatana na Menejimenti ya Wizara ya Maji na Wakurugenzi wa amefika mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kuwasilisha taarifa ya Hali ya huduma ya Maji katika Majiji nchini ambayo ni ARUSHA (AUWSA), DAR ES SALAAM (DAWASA), MWANZA (MWAUWASA), TANGA (TANGAUWASA), MBEYA (MBEYAUWSA), DODOMA (DUWASA)

Kamati ya Kudumu ya Bunge imetoa maoni yake kwa Wizara ya Maji baada ya kupokea taarifa hii ambapo imeanza kwa kueleza namna gani inaridhishwa na utendaji kazi wa Mamlaka hizo za Maji zilizowasilusha taarifa leo tarehe 20 Aug 2024 na kushauri maeneo mbalimbali yanayohitaji kufanyiwa maboresho hususani eneo la huduma kwa wateja, upotevu wa Maji, makusanyo ya madeni na utekelezaji wa Miradi.

Akihitimisha hoja za wajumbe wa Kamati ya Maji na Mazingira Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amesema wizara inakwenda kufanyia kazi ushauri, maoni, maboresho na hoja za wajumbe katika kuhakikisha Mamlaka za Maji za Majiji zinaboresha na kuimarisha utendaji kazi wake na kutoa huduma ya uhakika ya Maji kwa wananchi.