Mbunge wa Arumeru aishukuru Serikali kwa kupeleka maji Mlangalini.
Kufuatia swali lililoulizwa na Mbunge wa Arumeru Magharibi Mhe. Noah mnamo tarehe 10/11/2023 "kwamba kutokana na kuongezeka Kwa idadi kubwa ya watu katika kijiji Cha kiserian kata ya mlangarini na kupelekea kuwepo Kwa upungufu wa maji je Serikali haioni haja ya kupeleka maji ya dharura hasa katika shule ya msingi Muungano Ili kunusuru wale watoto dhidi ya mgonjwa ya mlipuko kama U.T.I na kipindupindu "
Serikali baada ya kusikia maombi hayo ya Mhe Mbunge, Naibu waziri wa maji Mhe. Maryprisca Mahundi (MB) Aliagiza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha- AUWSA kuhakikisha maji yanafika katika shule ya msingi Muungano kijiji Cha kiserian kata ya mlangarini
Mnamo tar 14 Novemba 2023 Mhe. Mbunge Amekabidhiwa vifaa ikiwemo mabomba, ambayo yatahakikisha wananchi wa jirani na shule wanapata maji na shule mzima Kwa ujumla kupata maji ambapo kazi hiyo inatarajia kukamilika Tarehe 17 Novemba 2023.