MKUU WA WILAYA YA LONGIDO KWENYE MKUTANO NA WANANCHI WA KATA YA ORIENDEKE
MKUU WA WILAYA YA LONGIDO KWENYE MKUTANO NA WANANCHI WA KATA YA ORIENDEKE
Imewekwa: 20 December, 2023
Tarehe 19.12.2023 Mkuu wa Wilaya ya Longido amefanya mkutano na wananchi wa Kata ya Oriendeke kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili. Miongoni mwa changamoto ikiwa ni upatikanaji wa huduma ya majisafi kwa kitongoji cha Lesoiti kinachohudumiwa na AUWSA ambapo Mh DC ametolea ufafanuzi kuwa ujenzi wa bomba kubwa la kutoa maji ya kisima kilichopo Kata ya Sinya Kuja Tank la Namanga utakapokamilika tatizo la maji litaisha katika maeneo yanayohudumiwa na AUWSA yaliyopo katika Kata ya Oriendeke.