Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha

( AUWSA )

KIKAO CHA NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI NA WATUMISHI WA SEKTA YA MAJI MKOA WA ARUSHA

Imewekwa: 13 June, 2024
KIKAO CHA NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI NA WATUMISHI WA SEKTA YA MAJI MKOA WA ARUSHA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Bi. Agnes K. Meena amefanya kikao kazi na Menejimenti za Watumishi wa Sekta ya Maji wa Mkoa wa Arusha ambao ni RUWASA, AUWSA, Bonde la Pangani pamoja na Maabara ya Mkoa wa Arusha. 

Katika kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu amewasii watumishi wa Sekta ya Maji kutokua kikwazo katika swala la kumtua mama ndoo kichwani. “Hakuna  Miujiza katika kutenda kazi. Kila mtu katika nafasi yake afanye kazi kwa bidii na kwa ushirikiano kwani bila ushirikano mambo hayataenda.” 

Pia Naibu Katibu Mkuu ameagiza menejimenti za Sekta ya maji kufanyia kazi changamoto za Wateja kwa wakati ili kuhakikisha kero za maji zinapungua kwenye jamii tunapotoa huduma.

Mwisho, amewaagiza watumishi wawe na mahusiano bora na wananchi/Wateja ,viongozi wa serekali na chama ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa sahihi kwa wakati za upatikanaji wa huduma ,alisisitiza mahusiano ni msingi mzuri wa kufanya kazi kwa ubora.