Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha

( AUWSA )

AWESO ATOA MATUMAINI MAKUBWA MONDULI,KAZI KUBWA INAFANYIKA SEKTA YA MAJI

Imewekwa: 31 January, 2024
AWESO ATOA MATUMAINI MAKUBWA MONDULI,KAZI KUBWA INAFANYIKA SEKTA YA MAJI

Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso akiwa njiani kuelekea jiji la Arusha kutekeleza agizo la chama ameshiriki katika Ziara ya Katibu Itikadi, uenezi na mafunzo CCM Ndug. Paul Makonda Wilayani Monduli Mkoani Arusha ambapo amepata fursa ya kueleza utekelezaji na hali ya upatikanaji wa huduma ya Majisafi na salama wilayani hapo.

Waziri Aweso ameeleza kuwa mpaka sasa Wizara imesani mikataba miwili yenye thamani ya zaidi Bilioni 27 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kupeleka maji maeneo yote yenye changamoto na kumaliza kabisa tatizo la maji katika wilaya ya Monduli.

Aidha Akiwa eneo la Makuyuni amesisitiza kuwa Mpango ulioko ni mradi wa Vijiji 4 Makuyuni, Naiti, Mbuyuni na Losimingori wenye thamani ya Bilion 7 ambao utazalisha maji lita 1,200,000 na kunufaisha wananchi 20,613.

Pia, Aweso amesisitiza uwepo wa Mradi wa maji Vijiji 13 wenye gharama ya Tshs Bilioni 20.