AUWSA YACHANGIA WAHANGA WA MAFURIKO HANANG
AUWSA YACHANGIA WAHANGA WA MAFURIKO HANANG
Imewekwa: 08 December, 2023
7 Disemba 2023.
Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Watumishi wa Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA) wameungana na Watanzania wote katika kutoa Salamu za pole kwa kuchangia wahanga wa mafuriko Wilayani Hanang mkoa wa Manyara Matanki ya Kuifadhia MajiSafi yenye thamani ya Tsh. Milioni kumi katika Kijiji cha Gendabi ambapo usiku wa kuamkia tarehe 2 Disemba 2023 kulitokea mafuriko yaliyosababisha madhara makubwa ya vifo, uharibifu wa mali, makazi pamoja na miundombinu muhimu ikiwemo miundombinu ya Maji.