Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha

( AUWSA )

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)

Imewekwa: 14 November, 2023
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), ni taasisi ya udhibiti wa huduma za nishati na maji inayojitegemea, iliyoundwa kwa Sheria ya EWURA Sura ya 414 ya Sheria za Tanzania na marekebisho yake Na. 6 ya mwaka 2019.

EWURA, ilianza kazi rasmi Septemba, 2006 ikiwa na wajibu wa kusimamia shughuli zote za kiuchumi na kiufundi katika sekta za Nishati(umeme, petroli na gesi asilia); na Maji (majisafi na usafi wa mazingira).

Katika kutekeleza wajibu wake, kwa uwazi na kwa manufaa ya wote, EWURA inazingatia sheria za kisekta, sera na miongozo ifuatayo:-

Sera ya Taifa ya Nishati (2015), Sera ya Taifa ya Maji (2002), Sheria ya EWURA, Sura Na. 414; Sheria ya Umeme, Sura Na. 131; Sheria ya Petroli, Sura Na. 392; Sheria ya Maji na Usafi wa Mazingira, Sura Na. 279;  kanuni na miongozo  mbalimbali.