Mamlaka ya Serikali Mtandao
Mamlaka ya Serikali Mtandao
Imewekwa: 14 November, 2023
e-GA inakusudia kutekeleza afua mbalimbali ili kusaidia taasisi za umma kutoa huduma mtandao kwa ufanisi. Utekelezaji huo utafanyika kwa kufanya yafuatayo:
- Uongezaji na uboreshaji wa njia za utoaji wa huduma za serikali mtandao
- Utoaji wa huduma za ushauri na msaada wa kiufundi
- Uboreshaji wa uwezo wa rasilimaliwatu katika taasisi,
- Uwezeshaji wa upatikanaji wa miundombinu na mifumo salama na ya kuaminika ya Serikali mtandao
- Uimarishaji na uratibu wa jitihada za usalama wa kimtandao katika taasisi za umma.