Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha

( AUWSA )

MKUTANO WA WADAU SEKTA YA MAJI TAREHE 13–14 DECEMBER 2023

Imewekwa: 12 December, 2023
MKUTANO WA WADAU SEKTA YA MAJI TAREHE 13–14 DECEMBER 2023

AICC,ARUSHA

Wizara ya Maji inawaalika katika mkutano wa wadau wa sekta ya maji utakaofanyika tarehe 13 – 14 Desemba, 2023 katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Dhumuni kuu la mkutano huo ni Mheshimiwa Waziri wa Maji kuwashukuru wadau mbalimbali wa sekta kwa mchango wao mkubwa wa hali na mali katika kuwezesha mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya maji nchini.

Mgeni rasmi ni Mhe. Jumaa Hamidu Aweso (Mb), Waziri wa Maji.
Sambamba na hilo, wadau watapewa fursa ya kujadili, kutoa maoni na mapendekezo kwenye Rasimu ya Sera ya Taifa ya Maji ya Mwaka 2002 Toleo la Mwaka 2023 na Mpango Mkakati wa Wizara.