TAARIFA KWA UMMA KUHUSU WIZI WA MAJI

AUWSA inawatangazia Wananchi wote wa Jiji la Arusha kuwa ni kosa kisheria kushiriki katika vitendo vya wizi wa maji, kuchepusha mita au kujiunganishia tawi la maji bila kufuata taratibu za AUWSA Sheria ya maji na usafi wa mazingira Namba 5 ya mwaka 2019 kifungu cha 64 inaeleza

“ Kosa la kuchezea dira ya maji ili kufanya udanganyifu wa huduma ya maji uliyoomba adhabu yake ni faini kuanzia shilingi laki tano hadi milioni kumi au kifungo cha miezi sita hadi miaka miwili”

Hivyo Mwananchi jiepushe na vitendo vyovyote vya kuhujumu dira za maji, kuchepusha dira au kujiunganishia maji kinyume na taratibu zilizowekwa. AUWSA imetoa muda wa wiki moja kuanzia Tarehe 23/11/2020 hadi Tarehe 29/11/2020 kwa wale wote wenye makosa ya wizi wa maji, kuchepusha dira, wafike ofisi za AUWSA ili kurasimisha matawi yao. Baada ya kipindi hicho AUWSA kwa kushirikiana na vyombo vya sheria watafanya msako wa nyumba kwa nyumba ili kubaini watuhumiwa wote wa vitendo vya hujuma dhidi ya miundombinu na wezi wa maji.