Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ametembelea na kukagua mradi wa kuondoa majitaka katika jiji la Arusha uliopo eneo la Maskilia mkoani Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ametembelea na kukagua mradi wa kuondoa majitaka katika jiji la Arusha uliopo eneo la Maskilia mkoani Arusha. Mradi huo una uwezo wa kutibu majitaka lita milioni 22 kwa siku ukiwa ni sehemu ya mradi mkubwa wa maji wa bilioni 520 unaotarajiwa kuwapatia maji safi na salama wakazi wa  mkoa wa Arusha.

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo, Makamu wa Rais ameitaka wizara ya maji  kutumia mradi huo wa majitaka kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji ili kuwasaidia wananchi wa eneo la Maskilia na maeneo jirani. Ameitaka wizara kutafuta teknolojia rafiki kupitia shirika la kimataifa la mazingira (UNEP) itakayowezesha uchakataji wa maji hayo kwaajili ya kilimo. Amesema mradi huo utaongeza ajira pamoja na kuongeza uzalishaji katika kilimo.

Makamu wa Rais amezungumza na wananchi wa mtaa wa  Maskilia ambao wamemueleza changamoto ikiwemo ukosefu wa majisafi na salama pamoja na changamoto ya umeme na barabara. Makamu wa Rais ameigiza wizara ya maji kushughulikia haraka changamoto ya maji safi katika eneo hilo.

Download/s File: